Mvutano wa kisiasa waibuka kuhusu msamaha wa kisheria wa Waziri Mkuu wa Israel.
Donald Trump ametoa kauli kali dhidi ya Rais wa Israel Isaac Herzog, akidai kuwa alimdanganya kuhusu uwezekano wa kumsamehe Benjamin Netanyahu anayekabiliwa na mashtaka ya ufisadi.
Trump alieleza kuwa kesi hiyo inapaswa kuwekwa pembeni ili kumruhusu Netanyahu kuangazia masuala ya vita na usalama wa taifa. Hata hivyo, upande wa Israel umesisitiza kuwa mchakato wowote wa msamaha unafuata sheria na hauwezi kufanywa kwa shinikizo la kisiasa.
Wakati huo huo, mvutano wa kijeshi kati ya Israel na Iran unaendelea, ukiongeza presha kwa viongozi wa eneo hilo.
CHANZO: Newstimehub