Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais Donald Trump alimueleze mtangazaji wa kipindi cha MS NOW, Joe Scarborough, kwamba Marekani inapanga “kuchukua mafuta,” kufuatia mashambulizi yaliyofanyika nchini Venezuela na kukamatwa kwa Nicolás Maduro.

Trump amesema Marekani itachukua mafuta ya Venezuela

Rais Donald Trump wa Marekani amesema katika mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha MS NOW, Joe Scarborough, kwamba operesheni ya kijeshi iliyomkamata Maduro ilitekelezwa kwa ufanisi wa hali ya juu.

Rais Donald Trump alimueleze mtangazaji wa kipindi cha MS NOW, Joe Scarborough, kwamba Marekani inapanga “kuchukua mafuta,” kufuatia mashambulizi yaliyofanyika nchini Venezuela na kukamatwa kwa Nicolás Maduro.

Mtangazaji huyo anasema kuwa alipomhoji Trump kuhusu wazo la Marekani kuiendesha Venezuela, akilinganisha hali hiyo na uvamizi wa Iraq uliofanywa wakati wa rais George W. Bush, Trump alisema, "‘Joe, tofauti kati ya Iraq na hii ni kwamba, Bush hakuchukua mafuta. Sisi tutachukua mafuta."

Mtangazaji huyo wa MS NOW alisema Trump alizungumza waziwazi bila kuweka masharti ya kunukuliwa, na akamnukuu rais akisema: “Mwaka 2016 nilisema tulipaswa kuchukua mafuta. Ilisababisha mabishano makubwa. Lakini ukweli ni kwamba tulipaswa kuyachukua.”

“Tutajenga upya miundombinu yao ya mafuta iliyoharibika, na safari hii tutachukua mafuta,” Trump alisema, kwa mujibu wa Scarborough.

Wakati huo huo, Trump alisema siku ya Jumatatu ya kwamba, Serikali ya mpito ya Venezuela itaikabidhi Marekani kati ya mapipa milioni 30 hadi 50 ya mafuta yaliyo chini ya vikwazo.

“Mafuta tutakayopokea kutoka Venezuela yatauzwa kwa bei ya soko, na mimi, kama Rais wa Marekani, nitasimamia moja kwa moja usimamizi wa mapato yake,” aliongeza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#