Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Sudan ina matumaini kuwa ushindi dhidi ya Senegal katika Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumamosi unaweza kuchochea usitishaji wa mapigano nchini humo, au hata kuleta amani ya muda mrefu, alisema kocha Kwesi Appiah siku ya Ijumaa.
Timu ya Sudan imefika hatua ya mtoano ya mashindano hayo kwa mara ya pili tu tangu walipotwaa ubingwa mwaka 1970, licha ya kushinda changamoto kubwa za kuishi uhamishoni kutokana na vita.
Vita kati ya wanamgambo wa RSF dhidi ya jeshi la Sudan vimeanza tangu Aprili 2023, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, huku mamilioni wakilazimika kuyahama makazi yao, huku njaa kali ikienea nchini humo.
Licha ya mgogoro huo, timu ya taifa ya Sudan imeendelea kucheza ikiwa uhamishoni na, kinyume na matarajio, imefanikiwa kufuzu kushriki kwa michuano ya AFCON nchini Morocco, ambako watakutana na Senegal inayotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora mwishoni mwa wiki.
“Mara nyingi hujaribu kukwepa maswali haya kwa sababu hisia ni nzito sana,” alisema Appiah, akionyesha kutoridhishwa kwake na kuulizwa kwa swali hilo, akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu athari za vita kwa timu yake.
“Si jambo tunalopenda kulizungumzia, lakini tuna matumaini kwamba tukishinda, vita vitapoa au hata kusitishwa kabisa.”
Pande zinazopigana zimeshereka ushindi
“Kulikuwa na mechi moja tuliyoshinda (katika mechi za hivi karibuni za kufuzu Kombe la Dunia) ambapo vikundi vinavyopigana viliweka chini silaha zao na kila mtu alikuwa anasherehekea. Mpira unaweza kubadilisha mambo duniani,” aliongeza kocha huyo ambaye ni raia wa Ghana.
Sudan haijacheza mechi ya nyumbani kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita kutokana na uharibifu wa miundombinu ya soka. Klabu mbili kubwa nchini humo zimehamia Rwanda, ambako zinashiriki ligi ya huko kama wageni, na Al Hilal ya Khartoum pia imefika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.
“Kucheza ugenini na katika mazingira haya ambayo nyote mnayafahamu ni jambo gumu sana,” aliongeza kapteni wa timu hiyo Bakhit Khamis.
“Ni vigumu sana kwetu kuishi mbali na familia zetu, mbali na nyumba zetu. Tunajaribu kukabiliana na hali hizi, kuwafurahisha mashabiki wetu, na tunatumaini mambo yatakuwa bora. Kila tunachofanya uwanjani ni jaribio la kufanya mambo yawe bora kwa watu wetu,” alisema.
Comments
No comments Yet
Comment