Sport
Dollar
43,0297
0.16 %Euro
50,4667
-0.24 %Gram Gold
5.985,7300
0.33 %Quarter Gold
10.281,2400
1.21 %Silver
100,3300
1.41 %Kikosi cha RSF kimesema kuwa mshauri mkuu wa usalama wa kiongozi wake ameuawa pamoja na wasaidizi kadhaa katika shambulio la ndegee isiyo na rubani 'droni' karibu na mji wa Zalingei.
Hamid Ali Abubakar, mshauri wa usalama wa kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, aliuawa pamoja na wasaidizi wake kadhaa katika shambulio la droni lililotekelezwa na jeshi la Sudan karibu na mji wa Zalingei, mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kati. Taarifa hiyo ilithibitishwa na mshauri wa usalama wa RSF, Al Basha Tabiq.
Tabiq alitangaza kifo hicho kupitia chapisho kwenye mitandao ya kijamii. Vyanzo vya eneo hilo vilisema kuwa droni ilishambulia mkutano wa vikosi vya RSF katika kijiji cha Al Firdous, eneo la Waranga karibu na Zalingei, magharibi mwa Sudan.
Nafasi ya Abubakar
Vyanzo viliongeza kuwa Abubakar alikuwa mshauri wa karibu wa Dagalo na pia kamanda wa mapambano aliyekuwa anaongoza kikosi cha Al Saif Al Battar, ambacho kina mamia ya wapiganaji wa RSF. Aidha, alichukua nafasi muhimu katika kuhamasisha makabila na viongozi wa jadi kuiunga mkono RSF.
Hadi sasa, jeshi la Sudan halijatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo.
Majimbo matatu ya Kordofan — Kaskazini, Magharibi na Kusini — yameshuhudia wiki kadhaa za mapigano makali kati ya jeshi na RSF, hali iliyosababisha makumi ya maelfu ya watu kukimbia makazi yao.
Kati ya majimbo 18 ya Sudan, RSF inadhibiti majimbo yote matano ya eneo la Darfur magharibi mwa nchi, isipokuwa baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Darfur ya Kaskazini ambayo bado yako chini ya udhibiti wa jeshi. Kwa upande mwingine, jeshi linadhibiti sehemu kubwa ya majimbo 13 yaliyosalia kusini, kaskazini, mashariki na katikati mwa Sudan, ikiwemo mji mkuu, Khartoum.
Mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan umeendelea kuwa mbaya zaidi tangu vita kati ya jeshi na RSF vilipozuka Aprili 2023 kufuatia mzozo wa kuunganisha taasisi za kijeshi. Vita hivyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu na mamilioni kulazimika kuyahama makazi yao.
Comments
No comments Yet
Comment