Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tanzania Bara kwa kawaida, kila tarehe 9 Desemba huadhimisha Siku ya Uhuru, na mwaka huu taifa hilo linatimiza miaka 64 tangu lipate uhuru wake.

Tanzania yaadhimisha miaka 64 ya Uhuru huku kukiwa na hofu ya usalama

Tofauti na ilivyozoeleka ambapo siku ya kuadhimisha Siku ya Uhuru huwa na shamrashamra na furaha ya kitaifa, mwaka huu hali imekuwa tofauti.

Serikali imewashauri wananchi wake kuitumia siku hiyo kama sehemu ya mapumziko kwa kubaki majumbani, huku ikiwashauri wale tu wenye dharura ya kutoka kufanya hivyo.

Kufuatia hofu ya kuibuka kwa vurugu, idadi kubwa ya wananchi hasa katika miji mikubwa wameamua kubaki majumbani, hivyo kuacha sehemu kubwa ya miji kama Dar es Salaam bila watu barabarani. 

Hatua hii imechukuliwa kufuatia kuwepo kwa wito wa maandamano yaliyopangwa yenye lengo la kudai mabadiliko ya kiutawala huku yakipinga serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo, serikali imewatahadharisha wananchi wake dhidi ya kushiriki maandamano hayo na kusema sio halali.

Leo ikiwa ni siku ya 40 tangu 29 Oktoba, ambapo Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu, ambapo baadae ulikumbwa na vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi ambao mpaka leo idadi kamili haifahamiki.

Licha ya polisi kulaumiwa kwa kutumia nguvu iliyopitiliza, Rais Samia, amewatetea polisi kwa kusema kuwa vikosi vya usalama vililazimika kutumia “nguvu muafaka” kukabiliana na waandamanaji aliowataja kuwa hawakuwa na nia ya amani.

Wakati hayo yakiendelea, mataifa kadhaa ya Magharibi yametoa wito kwa Tanzania kuheshimu haki za binadamu na kulinda uhuru wa kujieleza.

Pamoja na mvutano uliopo, Rais Samia ametangaza wito wa maridhiano yasiyokuwa na masharti.

Hata hivyo, bado haijafahamika wazi iwapo upinzani utakubali kuketi meza moja na serikali, na kama wakikubali, mazungumzo hayo yatafanyika chini ya mazingira gani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#