Sport
Dollar
42,4521
0.01 %Euro
49,6670
0.22 %Gram Gold
5.742,9700
0.04 %Quarter Gold
9.512,2800
-0.25 %Silver
77,8300
-2.52 %Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA), bei za mafuta ya petroli na ya taa, zimeendelea kushuka kutokana na kupungua kwa gharama za uagizaji kwa yale yaliyopitia bandari ya Dar es Salaam.
Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania (EWURA) imetangaza punguzo la gharama ya nishati ya petroli kwa mafuta yenye kupitia bandari ya Dar es Salaam.
Kulingana na taarifa yake iliyotolewa Desemba 3, 2025, kwa sasa, lita moja ya petroli inayopitia bandari ya Dar es Salaam, itauzwa kwa Dola 1.13 (Shilingi za Kitanzania 2,749) kutoka shilingi za Kitanzania 2,752.
“Bei za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zinazingatia gharam za mafuta yalisafishwa katika soko la nchi za Kiarabu.
Katika bei kikomo kwa Desemaba 2025, bei za mafuta katika soko la dunia zimeongezeka kwa asilimia 1.7 kwa petroli, asilimia 4.8 kwa dizeli na asilimia 6.4 kwa mafuta ya taa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo, pia ilibainisha kuwa, bei ya rejareja ya petroli imepungua kwa shilingi 2.38 (Dar es Salaam), 2.26 (Tanga) na shilingi 2.45 kwa Mtwara.
Aidha, bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam imepungua kwa shilingi 120.48 ikilinganishwa na bei za mwezi Novemba 2025.
Mamlaka hiyo imewahimiza wauzaji wa mafuta nchini humo, kutoa stakabadhi za mauzo kwa wanunuzi zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita, kwani stakabadhi hizo hutumika kama kithibiti kunapokuwa na changamoto yoyote kuhusu huduma hiyo.
Comments
No comments Yet
Comment