Sport
Dollar
42,4521
0.01 %Euro
49,6670
0.22 %Gram Gold
5.742,9700
0.04 %Quarter Gold
9.512,2800
-0.25 %Silver
77,8300
-2.52 %Kanuni ya 11 ya uendeshaji wa shughuli za EAC, unataka akidi za nchi zote wanachama zitimie, ili Mkutano wa Wakuu wa EAC ufanyike.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)imeahirisha mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Desemba 6, 2025 jijini Nairobi nchini Kenya.
Mshauri wa masuala ya mawasiliano ndani ya EAC, Lilian Kiarie aliithibitishia TRT Afrika taarifa za kuahirishwa kwa kikao hicho, japo hakuingia kwa undani sababu za uamuzi huo.
Hatua hiyo inakuja wakati wa uwepo wa taarifa za maandamano ya amani nchini Tanzania, yaliyoratibiwa kufanyika Desemba 9, 2025.
Kanuni ya 11 ya uendeshaji wa shughuli za EAC, unataka akidi za nchi zote wanachama zitimie, ili Mkutano wa Wakuu wa EAC ufanyike.
Kati ya ajenda ambazo zilipangwa kujadiliwa kwenye mkutano huo wa Nairobi, ni pamoja na uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo.
Hili linakuja wakati uenyekiti wa rais wa Kenya, William Ruto ukifikia ukingoni, huku Rais Hassan Sheikh Mohamud akitarajiwa kumrithi.
Comments
No comments Yet
Comment