Sport
Dollar
40,5962
0.02 %Euro
46,5344
0.41 %Gram Gold
4.296,0200
0.52 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mpaka huo haujafafanuliwa vizuri na mara nyingi huzua mapigano madogo madogo
Takriban watu sita wameuawa katika mapigano kati ya majeshi ya Sudan Kusini na Uganda karibu na mpaka wao wa pamoja.
Mpaka huo haujafafanuliwa vizuri na mara nyingi huzua mapigano madogo madogo.
Wanajeshi hao wawili walirushiana risasi Jumatatu katika kaunti ya Kajo Keji, Sudan Kusini, na kupelekea kuuawa kwa wanajeshi watano wa jeshi la Sudan Kusini (SSPDF), maafisa wa Sudan Kusini walisema.
Msemaji wa Jeshi la Uganda Felix Kulayigye alisema wanajeshi wa SSPDF waliingia katika eneo la Nile Magharibi nchini Uganda na kukataa kuondoka, na kusababisha mapigano ya bunduki, ambapo mwanajeshi mmoja wa Uganda alifariki.
Uganda imeunga mkono vikosi vya jeshi la taifa ya Sudan Kusini kwa miongo kadhaa, na kusaidia nchi hiyo kupigania uhuru, ambao ulipatikana mwaka 2011, na wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuata.
Kaunti ya Kajo-Keji ilisema katika taarifa kwamba wanajeshi watano wa SSPDF wameuawa katika shambulio la ghafla la vikosi vya Uganda vinavyoungwa mkono na vifaru na mizinga.
Jeshi la Sudan Kusini limethibitisha kutokea kwa mapigano hayo lakini halikutaja idadi ya waliofariki.
“Kamati iliyopo ya pamoja ya mpaka itaangalia njia za kupata suluhu la amani kwa mizozo ya mara kwa mara inayohusiana na mpaka,” msemaji wa SSPDF Lul Ruai Koang alisema katika taarifa iliyotolewa Jumanne jioni.
Mwezi Machi, Sudan Kusini ililialika jeshi la Uganda kusaidia kuimarisha usalama katika mji mkuu wa Juba, kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kutokana na msukosuko kati ya Kiir na mpinzani wake, Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar.
Comments
No comments Yet
Comment