Dollar

43,0297

0.16 %

Euro

50,4667

-0.24 %

Gram Gold

5.985,7300

0.33 %

Quarter Gold

10.281,2400

1.21 %

Silver

100,3300

1.41 %

Nafasi ya uenyekiti inayozunguka ilianza kutekelezwa tarehe 1 Januari 2026.

Somalia kuongoza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Somalia imechukua rasmi uenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hatua muhimu katika kuongezeka kwa umaarufu wake duniani.

Nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inatarajiwa kuongoza masuala ya Baraza la Usalama kwa mwezi wa Januari, ikiongoza vikao na ajenda ya kazi ya chombo hicho, chenye jukumu la kudumisha amani na usalama vya kimataifa.

Uenyekiti wa Somalia katika Baraza la Usalama utaongozwa na Mwakilishi wake wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Abukar Osman, akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Samuel Žbogar wa Slovenia.

Katika taarifa, ujumbe wa Somalia kwenye UN ulisema kuwa, wakati wa uenyekiti wake, Somalia itakuza "mazungumzo ya kujenga na ya kujumuisha.”

Amani ya kimataifa

Ilisema kuwa inaongozwa na "wajibu wa kudumisha amani na usalama wa kimataifa" na kwamba itatoa kipaumbele katika "mbinu za kazi za uwazi, zenye ufanisi, na zinazotokana na makubaliano."

Uteuzi wa Somalia kushika nafasi hiyo katika Baraza la Usalama la UN lenye wanachama 15 akiwa mwanachama asiye wa kudumu.

Liberia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nchi nyingine za Afrika zilizochaguliwa kwa muhula wa miaka miwili, kuanzia 1 Januari 2026.

Licha ya umuhimu wake, uwepo wa nchi za Afrika kama wanachama wasio wa kudumu haukidhi mahitaji ya bara hilo.

Kura ya turufu

Kwa miongo kadhaa, nchi za Afrika zimetaka nafasi ya kudumu yenye uwezo wa kura ya turufu, na kukosoa mpangilio uliopo sasa kwamba 'haufai' kwa bara hilo.

Nchi tano pekee zilizo na viti vya kudumu na uwezo wa kura ya turufu katika Baraza la Usalama ni: Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, na China.

Hii ni mara ya kwanza kwa Somalia kushika uenyekiti wa Baraza la Usalama la UN tangu mwaka 1971, yaani baada ya miaka 55.

Maendeleo haya ya hivi karibuni yanaonekana na wachunguzi kama ishara nyingine thabiti ya kuibuka tena kwa nchi hiyo kufuatia miaka ya migogoro ya ndani na majanga ya asili.

Hata hivyo, yanakuja katika wakati mgumu katikati ya mvutano kati ya Somalia na Marekani, ambapo serikali ya Trump imekuwa ukilenga watu wenye asili ya Kisomali waliopo nchini Marekani.

Vivyo hivyo, kumekuwa na hasira ya kimataifa hivi karibuni baada ya Israel kutangaza kulitambua rasmi eneo la Somalia la Somaliland kama taifa huru, huku Somalia ikisema hatua hiyo ni kinyume na uhuru wake wa kitaifa na uadilifu wa mipaka yake.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#