Senegal imekosoa uamuzi wa CAF uliyoipa Morocco ushindi wa mezani baada ya tukio la wachezaji kutoka uwanjani.
CAF imetangaza rasmi Morocco kuwa mabingwa wa AFCON baada ya kubadilisha matokeo ya fainali dhidi ya Senegal kuwa 3-0.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia tukio la wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani wakipinga penalti iliyotolewa kwa Morocco katika dakika za mwisho za mchezo.
Nahodha Sadio Mane aliwashawishi wachezaji kurejea uwanjani, lakini CAF ilisema kitendo hicho kilikiuka kanuni za mashindano.
Senegal sasa imeapa kupinga uamuzi huo mahakamani, ikisema unaharibu hadhi ya soka barani Afrika.
CHANZO: Newstimehub