Dollar

39,1563

0 %

Euro

44,7470

0.4 %

Gram Gold

4.220,6900

-0.03 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Machi 2025, wanaharakati nchini Rwanda walitoa wito wa kuchukua hatua kali zaidi za serikali ili kuongeza msaada wa kisheria kwa watoto wanaotuhumiwa kwa uhalifu, wakihimiza marekebisho ya haraka ili kuboresha mchakato wa mahakama kwa watoto wadogo.

Rwanda yakabiliwa na changamoto ya ongezeko la uhalifu kwa watoto

Chama cha Wanasheria cha Rwanda (RBA) kinasema kuwa idadi ya watoto wahalifu imeongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Uhalifu wa watoto unafanywa na watu walio chini ya umri wa miaka 18.

"Katika miaka minne iliyopita, kutoka 2020 hadi 2024, katika takwimu zetu za Chama cha Wanasheria, idadi ya wale ambao tuliweza kuwawakilisha ilitoka 2,000 hadi 4,500 hivi," Moise Nkundabarashi, Rais wa RBA, alisema katika mkutano na wanasheria.

Naye Mhadhiri wa Haki za Watoto wa Taasisi ya Sheria na Maendeleo (ILDP) Naomi Umuhoza ambaye ni kati ya watetezi wa haki amesisitiza kuwa kuna familia ambazo hazitekelezi wajibu wake.

“Watoto ni wachanga, wanaharibiwa na mazingira, mtoto hafai kufika kiwango cha kufikishwa mahakamani. Familia ina jukumu kubwa katika kulea watoto ipasavyo, jamii pia iingilie kati pale inapotokea uzembe wa familia katika kuwaadhibu watoto ili kupunguza uhalifu kwa watoto wadogo,’’ alisema Umuhoza.

Yannick Boris, mwanafunzi katika mpango wa Haki ya Watoto katika ILPD, alisema,

"Kuna mipango tofauti, sheria za ulinzi wa mtoto kuhusu haki ya watoto ambazo zimetengenezwa. Familia ikiwa chimbuko la tabia na nidhamu, kila mtu katika jamii anapaswa kuwajibika, linapokuja suala la kumlinda mtoto."

Machi 2025, wanaharakati nchini Rwanda walitoa wito wa kuchukua hatua kali zaidi za serikali ili kuongeza msaada wa kisheria kwa watoto wanaotuhumiwa kwa uhalifu, wakihimiza marekebisho ya haraka ili kuboresha mchakato wa mahakama kwa watoto wadogo.

"Lazima tushughulikie ucheleweshaji wa mfumo wa haki na kuhakikisha kuwa watoto wanapata uwakilishi ufaao," alisema Seneta Adrie Umuhire, rais wa Tume ya Haki za Kibinadamu.

Alikiri baadhi ya maendeleo chanya, kama vile uanzishwaji wa sheria za kulinda watoto, lakini alisisitiza kuwa bado kuna changamoto kubwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#