Sport
Dollar
39,1259
-0.06 %Euro
44,7942
0.48 %Gram Gold
4.225,2200
0.08 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%‘Jaribio la wapiganaji magaidi’ kutaka kuingia katika kambi ya jeshi ya Timbuktu lilitibuliwa, na hali sasa imetulia na ‘imedhibitiwa,’ Jeshi la Mali lilisema
Siku ya Jumatatu jeshI la Mali lilisema limefanikiwa kutibuwa “jaribio la magaidi” la kutaka kuvamia kambi ya kijeshi ya Timbuktu kaskazini mwa Mali.
Magaidi kumi na tatu “walikatwa makali,” na silaha, magari na vitu vingine vilipatikana, taarifa hiyo ya jeshi ilisema.
Ilisema kuwa hali kwa sasa “imedhibitiwa” na juhudi za kuwasaka zinaendelea kote mjini Timbuktu.
Taarifa hiyo haikutaja kundi la kigaidi ambalo limehusika na jaribio hilo, lakini wapiganaji wote wenye uhusiano na makundi ya ISIS (Daesh) na al-Qaeda wamewahi kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo siku za nyuma.
Haya yamejiri siku moja baada ya shambulio la magaidi kulenga kambi ya kijeshi ya Boulkessi katikati mwa eneo la Douentza.
Comments
No comments Yet
Comment