Sport
Dollar
41,9827
0.02 %Euro
48,6641
-0.13 %Gram Gold
5.457,2300
-1.98 %Quarter Gold
9.445,7600
-4.91 %Silver
64,9100
-1.32 %Shambulizi hilo linakuja siku moja kabla ya kufunguliwa tena kwa uwanja huo wa Sudan kwa ajili ya safari za ndege za nyumbani baada ya kufungwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Wapiganaji wa RSF wameshambulia kwa ndege zisizokuwa na rubani maeneo muhimu katika mji mkuu wa Sudan, wakilenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum na kituo cha kufua umeme.
Walioshuhudia wanasema kuwa shirika la habari la Rakoba News Jumanne lilisema kuwa milipuko isiyopungua minane ilisikika ndani na karibu ya uwanja wa ndege, ambapo Mamlaka ya Safari za Anga ilikuwa imepanga kufungua tena kwa ajili ya safari za ndani siku ya Jumatano, ikiwa ni ya kwanza tangu mapigano kuanza karibu miezi 30 iliyopita.
Mashambulizi hayo yanaonekana kutatiza kuanzishwa huko kwa safari kulikokuwa kunasubiriwa kwa muda mrefu, shirika hilo lilisema.
Ndege kadhaa zisizo na rubani ziliangushwa
Jeshi la Sudan linasemekana kuziangusha ndege kadhaa zisizokuwa na rubani, lakini zingine zilifanikiwa kushambulia, kusababisha madhara na wasiwasi katika maeneo ya karibu.
Jeshi wala RSF hawajazungumzia lolote kuhusu taarifa hizo.
Jeshi la Sudan lilitangaza mwezi Machi kuchukuwa udhibiti wa uwanja wa ndege wa Khartoum na maeneo ya karibu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita kati ya pande hizo mbili Aprili 2023.
Comments
No comments Yet
Comment