Hofu ilitanda katika hafla ya White House correspondents’ dinner baada ya risasi kusikika karibu na eneo la tukio.

Risasi Zasababisha Taharuki Katika Dinner ya White House, Trump Aokoka

Hofu ilitanda katika hafla ya White House correspondents’ dinner baada ya risasi kusikika karibu na eneo la tukio.

Rais Donald Trump pamoja na viongozi wengine waliondolewa haraka na walinzi wake huku hali ya taharuki ikizuka ndani ya ukumbi.

Mshukiwa aliyekuwa na silaha alikamatwa na maafisa wa usalama kabla ya kufanikiwa kuingia ndani ya ukumbi mkuu.

Ripoti zinaonyesha kuwa afisa mmoja wa usalama aliguswa na risasi lakini alinusurika kutokana na kuvaa vifaa vya kujilinda.

Tukio hilo limeibua wasiwasi kuhusu usalama wa hafla kubwa za kisiasa nchini Marekani

Chanzo: Newstimehub 

#