Sport
Dollar
43,0519
0.03 %Euro
50,3405
0.07 %Gram Gold
6.135,3300
-0.39 %Quarter Gold
10.302,3900
-0.93 %Silver
103,1400
-4.81 %Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Rais Faustin-Archange Touadera ameshinda muhula wa tatu wa urais baada ya kuondolewa kwa kikomo cha mihula ya uongozi.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi, Rais Touadera amepata ushindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita, akijipatia asilimia 76.15 ya kura zote.
Touadera alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na baadaye akachaguliwa tena mwaka 2020, ambapo alipata asilimia 53.16 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi.
Uchaguzi huo ulifanyika kufuatia kura ya maoni ya katiba iliyofanyika mwaka 2023, ambayo iliondoa kikomo cha mihula ya urais na kuongeza muda wa muhula wa rais kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Hatua hiyo ilimruhusu Touadera kugombea kwa muhula wa tatu.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 68, ambaye awali alikuwa profesa wa somo la hisabati, alijenga kampeni yake juu ya kile alichokitaja kuwa ni maboresho katika hali ya usalama nchini.
Waangalizi wa kimataifa, wakiwemo Umoja wa Afrika na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSCA), walisema siku ya kupiga kura kulikuwa na amani kwa kiasi kikubwa, licha ya kuwepo kwa changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi.
Hata hivyo, muungano mkuu wa vyama vya upinzani unaojulikana kama Republican Bloc for the Defence of the Constitution ulisusia uchaguzi huo, ukidai kuwa haukuwa wa haki.
Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi huo, wakiwemo mawaziri wakuu wa zamani Anicet-Georges Dologuele na Henri-Marie Dondra, waliishutumu serikali kwa kuweka vikwazo katika kampeni, ikiwemo kuzuia safari za wagombea kwenda maeneo ya mikoani.
Mahakama ya Katiba ina hadi tarehe 20 Januari kuthibitisha rasmi matokeo hayo au kutoa uamuzi kuhusu pingamizi lolote litakalowasilishwa.
Comments
No comments Yet
Comment