Sport
Dollar
38,8627
0.28 %Euro
43,5101
-0.09 %Gram Gold
4.051,3100
0.44 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mabao mawili ya mchezaji wa Nigeria Victor Osimhen katika kipindi cha pili yalimpa jumla ya magoli zaidi ya 34 ambayo ndiyo iliyokuwa rekodi iliyowekwa na mchezaji wa zamani wa Galatasaray Mario Jardel katika msimu wa 2000/01.
Victor Osimhen alifunga mabao mawili Jumatano usiku na kuvunja rekodi ya magoli mengi zaidi kufungwa na mchezaji wa nje nchini Uturuki katika msimu mmoja pamoja na kuisaidia Galatasaray kushinda kombe la Uturuki linalodhaminiwa na benki ya Ziraat baada ya kuifunga Trabzonspor 3-0.
Mabao mawili ya mchezaji wa Nigeria Victor Osimhen katika kipindi cha pili yalimpa jumla ya magoli zaidi ya 34 ambayo ndiyo iliyokuwa rekodi iliyowekwa na mchezaji wa zamani wa Galatasaray Mario Jardel katika msimu wa 2000/01.
Kulikuwa na hisia mbalimbali katika uwanja wa Gaziantep siku ya Jumatano wakati nahodha Fernando Muslera alipokabidhiwa kombe hilo na Rais wa shirikisho la soka la Uturuki (TFF) İbrahim Hacıosmanoğlu.
Wachezaji wa Trabzonspor na benchi la ufundi hawakuhudhuria sherehe hizo.

Galatasaray wanaweza wakachukuwa ubingwa wa pili nchini Uturuki iwapo watapata ushindi dhidi ya Kayserispor siku ya Jumapili, ambapo itakuwa ubingwa wao wa 25 katika ligi kuu ya Uturuki.
"Ningependa kusema hongera sana kwa timu nzima. Tumefurahi sana. Tumepambana kuanzia mwanzo hadi mwisho. Pia tungependa kuwashkuru mashabiki. Walikuwa imara kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mechi. Tulikuwa tunapigania mataji matatu, lakini hatukubahatika katika taji moja. Siku ya Jumapili tutapambana tupate taji lingine," Osimhen alisema baada ya mechi.
Wachezaji na benchi la ufundi walikabidhiwa medali zao na Waziri wa Vijana na Michezo Osman Aşkın Bak na Rais wa shirikisho la soka la Uturuki (TFF) İbrahim Hacıosmanoğlu.
Mchezaji bora wa mechi: Victor Osimhen
Comments
No comments Yet
Comment