Sport
Dollar
40,6910
0.06 %Euro
47,3116
0.04 %Gram Gold
4.413,8600
0.07 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Paul Makonda anawania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini, akiwa pia amehudumu kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha nchini Tanzania.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshinda kwenye kura za maoni za kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi wa Oktoba 2025.
Makonda alijizolea kura 9,056, ambayo ni sawa na asilimia 97.65 ya kura zote halali zilizopigwa.
Kupitia matokeo yaliyotangaza Agosti 4, 2025, jumla ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo 10,186 walishiriki mchakato huo, huku waliopiga kura wakiwa ni 9,276.
Wagombea wengine walioshiriki mchakato huo ni pamoja na Mustapha Said Nassoro aliyepata kura 83, Hussein Omar Gonga (kura 46), Ally Said Babu (kura 28), Aminatha Salash Toure (kura 26), Lwembo Mkwavi Mghweno (kura 16) na Jasper Augustino Kishumbua (kura 10).
Katika uchaguzi wa mwaka 2020, Makonda ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alishindwa kufurukuta katika kura za maoni kuwania Ubunge jimbo la Kigamboni kupitia CCM.
Matokeo ya Agosti 4, 2025, yanampa Makonda nafasi kubwa ya kushinda kiti cha ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Comments
No comments Yet
Comment