Sport
Dollar
40,6910
0.06 %Euro
47,2408
0.06 %Gram Gold
4.413,8800
0.07 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Uamuzi huo umetolewa Agosti 4, 2025, na kutangazwa na Ubalozi wa Marekani mjini Bujumbura.
Marekani imesitisha utoaji wa Viza kwa raia wa Burundi kwa madai ya ukiukwaji wa baadhi ya masharti.
Uamuzi huo unafuatia agizo lililotolewa na serikali ya rais Donald Trump, hususani katika sera za uhamiaji.
"Kuheshimu hati za kusafiria sio suala binafsi, ni suala la kitaifa."
"Kwa bahati mbaya, kutokana na ukiukwaji wa mara kwa mara wa taratibu za kuingia Marekani, tumesitisha kwa muda zoezi la utoaji viza kwa raia wa Burundi,” ilisomeka taarifa iliyowekwa kwenye ukurasa wa X wa ubalozi wa Marekani.
Iliongeza taarifa hiyo:"Ni vyema tuheshimu sheria hizo, kwa sababu kosa la mtu mmoja linaweza kugharimu taifa zima."
Kulingana na ripoti ya mwaka 2024, iliyotolewa na mamlaka za Marekani, zaidi ya asilimia 15 ya Warundi walipitisha muda wao wa kukaa nchini Marekani, ukilinganisha na raia wa Chad na Japan.
Comments
No comments Yet
Comment