Sport
Dollar
41,0175
0.18 %Euro
47,6760
0.06 %Gram Gold
4.404,8500
0.22 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Waliofukuzwa nchini humo walikuwa miongoni mwa washukiwa 792 wanaoaminika kuhusika na wizi wa mitandaoni waliokamatwa katika msako jijini Lagos.
Nigeria imewaondoa nchini raia wa kigeni 102 ikiwemo raia wa China 50 waliopatikana na hatia ya "ugaidi wa mitandaoni na utapeli wa mitandaoni", taasisi ya kupambana na ufisadi katika taifa hilo la Afrika magharibi ilisema siku ya Alhamisi.
Raia mmoja wa Tunisia pia alikuwa miongoni mwa wale waliotimuliwa tangu Agosti 15, Taasisi hiyo ya Kupambana na ufisadi wa Kiuchumi na Fedha (EFCC) ilisema kwenye taarifa, huku wengine zaidi wakitarajiwa kuondolewa katika siku chache zijazo.
Walioondolewa nchini humo walikuwa miongoni mwa washukiwa 792 waliokamatwa katika msako wakihusishwa na wizi wa mitandaoni katika mtaa wa kifahari wa Victoria Island, jijini Lagos Disemba iliyopita.
Watu wasiopungua 192 miongoni mwa wale waliokamatwa walikuwa raia wa kigeni, Wachina wakiwa 148, EFCC ilisema.
Wanatapeli watu
Comments
No comments Yet
Comment