Dollar

40,7015

0.02 %

Euro

47,2204

1.43 %

Gram Gold

4.394,9300

2.22 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Uturuki amelaani vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalesina huko Gaza.

Ni muhimu kwa ubinadamu kumaliza udhalimu wa Israel huko Gaza: Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti kumaliza udhalimu wa Israel dhidi ya Gaza na kutoa kipaumbele kwa ugawaji wa misaada kwenye maeneo yaliyokumbwa na majanga ya kibinadamu.

Akizungumza na wanahabari akiwa na rais wa Gabon Brice Oligui Nguema, Erdogan alisema,“Kipaumbele chetu ni kuhakikisha kuwa misaada ya kibinadamu inawafikia ndugu zetu wa Gaza.”

“Kama ubinadamu, tunapaswa kufanya kila liwezekanalo kumaliza udhalimu huu,” alisema.

Rais huyo wa Uturuki alilaani vikali mashambulizi yanayoendelea ya Israel dhidi ya raia wa Palestina, hususani kwa kushindishwa njaa na kuteswa huko Gaza.

“Kwa kila tone la dhamira, huruma na utu uko ukingoni kutokana na udhalimu huu,” alisema.

“Hatupaswi kukaa kimya wakati watoto wanaendelea kufa kwa njaa huku raia wanaotafuta chakula wakipigwa risasi kwa makusudi.”

Shinikizo dhidi ya Israel

Aliongeza kuwa, Uturuki itaendelea kuongeza juhudi za kidiplomasia kuongeza shinikizo dhidi ya Israel.

“Tutajitahidi kuiongezea Israel shinikizo katika siku sijazo ili isitishe janga la kibinadamu huko Gaza,” alisema, akisisitiza kuwa Uturuki inaendelea kuratibu suala hilo na washirika wake wa kimataifa.

Akiangazia mshikamano wa Uturuki kwa Wapalestina, aliongeza: “Tunataka ndugu zetu wa Gaza wasijisikie wapweke. Tutaendelea kuhakikisha kuwa amani ya kudumu inapatikana.”

Erdogan aliguswa na uungwaji mkono wa Palestina na nchi za Ulaya, akisema kuwa “zinatia moyo.”

 “Tunathamini sauti za Ulaya. Tunafurahishwa na kila hatua ya kutambua dola ya Palestina,” alisema.

Kauli yake inakuja wakati Gaza inaendelea kukabiliana na majanga ya kibinadamum ambapo zaidi ya Wapalestina 60,000 wameuwawa kuanzia Oktoba 7, 2023, huku wakikabiliwa na upungufu wa chakula, maji na vifaa vya matibabu.

 

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#