Emine Polat alijifunza namna ya kutengeneza mwanasesere wa kitre mwaka 2004 na kuwafundisha wanafunzi zaidi ya mia moja. Miaka kadhaa awali, kukutana kwake na mvulana aliekuwa bubu kulibadilisha muelekeo wa maisha yake.
Na Zeki Tarik Sarioglu
Kwa zaidi ya miongo miwili, Emine Polat amekuwa akiendeleza utamaduni wa Kituruki katika utengenezaji wa mwanasesere wa kitre.
Mbunifu huyo aliezaliwa Erzincan, ambaye amejifunza usanii huo mwaka 2004, amefundisha wanafunzi zaidi ya 100 na kutambuliwa kitaifa kwa mchango wake wa kuendeleza utamaduni wa Kituruki.
“Kwa mfano, kama natengeneza mwanasesere kutoka eneo la Bahari Nyeusi, nazingatia taswira ya mtu kutoka eneo la Bahari Nyeusi,” alisema. “Najaribu kufufua hali hiyo.”
Pamoja na kuwa utengenezaji wa mwanasesere ulimfanya akatambuliwa kitaifa, kukutana kwake na mvulana mmoja mapema miaka ya 1990 kulibadilisha muelekeo wake maishani.
Mwanzo mpya
Alizaliwa Erzincan mwaka 1952, Polat alimaliza masomo ya upili katika shule yake ya wasichana kabla ya kuendeleza mafunzo katika idara ya masuala ya sanaa.
Baada ya watoto wake kukuwa, aliamua kufanya kazi. Alikuwa na umri wa miaka 39 mwaka 1991, “Nilikuwa sijawahi kuona watu wenye matatizo ya akili,” alisema. “Nilikuwa sijawahi kuona hili.”
Kwanza hili lilimshangaza, Polat akihoji kama angeweza kuendelea kufanya kazi katika shule.
“Nilipoona watoto, nililia na kurudi nyumbani, nikisema siwezi kufanya hivi.”
Lakini baadaye ya mwezi mmoja akarudi tena, mtazamo ukawa umeanza kubadilika.
“Nikaanza kuamini kuwa wale watoto wanahitaji msaada,” alisema. “Ikawa mwanzo mpya maishani mwangu.”
Tukio moja shuleni humo limebaki kwenye kumbukumbu yake. Wakati wa Wiki ya Kuhamasisha kuhusu Ulemavu, mume wake Polat alinunua biskuti na vinywaji kwa watoto.
Miongoni mwa watoto kulikuwa na mvulana aliyeitwa Cenk ambaye alikuwa bubu.
“Watu walidhani kuwa huyo mtoto hawezi kufanya chochote,” Polat anasema. “Huwa bado nina hisia nikizungumzia kuhusu hilo.”
Siku iliyofuata, wakati Polat akikusanya biskuti hizo za watoto darasani, kukaonekana panya.
Hali hii iliimarisha dhamira ya Polat ya kuwasaidia watoto walio na ulemavu.
“Mtoto ambaye kila mtu anasema hawezi kuelewa chochote alinisaidia. Nikatambua kuwa mimi pia nahitaji kuwasaidia watotot hawa.”
Ujenzi wa shule
Polat aliendelea kufanya kazi na watoto wenye ulemavu, na mwaka 1995, akawasiliana na baadhi ya marafiki zake Cigli, wilaya iliyoko Izmir, kuhusu kuanzisha shirika.
“Nikauliza, ‘Mnaonaje mpango wa kuanzisha shirika?’ Walisema, ‘Bila shaka, tuko pamoja na wewe.’”
Mwezi Januari 2026, Polat alipewa tuzo, ishara ya kutambuliwa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya Uturuki kwa magwiji wa utamaduni na sanaa. Rais Recep Tayyip Erdogan alimkabidhi tuzo hiyo katika hafla jijini Ankara.
“Hii ni heshima kubwa kwangu,” alisema. “Nitaienzi furaha hii maisha yangu yote.”
Kutokana na kujifunza mwenyewe usanii huo na kuwafundisha wanafunzi zaidi ya 100, Polat anatarajia kuwa utamaduni utadumishwa.
“Natumai ubunifu wake utaendelea kuwepo, kuimarika na hata kufika mbali zaidi.”
TRT Afrika — TRT Afrika
Maisha & Maendeleo

