Licha ya kushuka nafasi mbili katika orodha ya Forbes, Mohammed Dewji bado ndiye tajiri zaidi katika Afrika Mashariki na Kati.
Takwimu mpya za jarida la Forbes zinaonyesha kuwa mfanyabiashara wa Tanzania Mohammed Dewji bado anaongoza utajiri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Katika orodha ya matajiri barani Afrika, Dewji ameshika nafasi ya 14 akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 2.1.
Kwa upande mwingine, mfanyabiashara wa Nigeria Aliko Dangote ameendelea kushika nafasi ya kwanza barani Afrika, huku mfanyabiashara wa Afrika Kusini Johann Rupert akifuata katika nafasi ya pili.
CHANZO: Newstimehub