Serikali ya Morocco yaona jengo jipya kama nyenzo muhimu ya kuvutia watalii zaidi kuelekea michuano ya Dunia.
Serikali ya Morocco imeeleza kuwa mnara mpya wa Mohammed VI Tower utakuwa kichocheo muhimu katika mkakati wake wa kuongeza idadi ya watalii kabla ya nchi hiyo kuandaa kwa pamoja Kombe la Dunia la FIFA 2030.
Maafisa wa utalii wanasema mnara huo utaisaidia Morocco kuimarisha hadhi ya miji ya Rabat na Salé, ambayo kwa kawaida imekuwa nyuma ya miji maarufu ya utalii kama Marrakech na Casablanca.
Tayari Morocco ndiyo nchi inayotembelewa zaidi na watalii barani Afrika, na serikali inalenga kutumia miradi ya kisasa kama huu mnara kuongeza mvuto wa taifa hilo kwa wageni wa kimataifa.
Wachambuzi wanaamini kuwa maendeleo hayo yanaweza kusaidia Morocco kunufaika na ongezeko la watalii wanaochagua maeneo wanayoona kuwa salama zaidi katika kipindi cha migogoro ya kikanda.