Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mhifadhi huyo alizaliwa na kukulia nchini Uingereza, ingawa muda mwingi wa kazi zake, alitumia akiwa Uganda, Tanzania na Kenya ambako ndipo yalipokuwa makazi yake hadi umauti ulipomkuta.
Mhifadhi wa wanyamapori na mazingira kutoka Scotland Iain Douglas-Hamilton, amefariki dunia.
Douglas Hamilton, ambaye alijipatia umaarufu kwa uhifadhi wa Tembo katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda amefariki dunia Disemba 8, 2025 jijini Nairobi, akiwa na umri wa miaka 83.
Mhifadhi huyo atakumbukwa kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa mapambano dhidi ya ujangili wa tembo katika eneo la Afrika Mashariki.
Kazi hiyo ilipelekea kupigwa marufuku kwa biashara haramu ya pembe za ndovu.
"Kazi yake iliweka misingi ya tafiti mbalimbali kuhusu wanyamapori, hasa tembo,” ilisema taasisi ya Save the Elephant kupitia taarifa yake.
Mhifadhi huyo alizaliwa na kukulia nchini Uingereza, ingawa muda mwingi wa kazi zake, alitumia akiwa Uganda, Tanzania na Kenya ambako ndipo yalipokuwa makazi yake hadi umauti ulipomkuta.
Comments
No comments Yet
Comment