Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa tahadhari kwa raia wake walioko nchini Tanzania kuwa makini kufuatia maandamano dhidi ya serikai yaliyopangwa kufanyika tarehe 9 Disemba.
Hata hivyo ubalozi huo kupitia mtandao wa X, umeongeza kwamba licha ya maandamano hayo kupangwa kufanyika tarehe 9 Disemba, huenda yakaanza mapema tarehe 5.
Aidha, ubalozi huo umesema yoyote anayepanga kusafiri nchini Tanzania, ajipange kwa usumbufu wa usafiri, ikiwemo safari za ndege njia za barabarani na baharini, na kuzimwa kwa mtandao wa intaneti pamoja na amri ya kutotoka nje.
Taarifa hiyo pia ilisema, kufuatia vurugu zilizoshuhudiwa nchini humo, vyombo vya usalama vimeanza kuwalenga raia wa kigeni wakisaka vifaa vya elektroniki vinavyosambaza ushahidi wa ghasia zilizotokea.
Polisi imetahadharisha ya kwamba kusambazwa kwa picha au video zitakazosababisha taharuki nchini ni uhalifu chini ya sheria ya Tanzania.
Comments
No comments Yet
Comment