Sport
Ghana imeanza uchunguzi baada ya madai kwamba baadhi ya watengenezaji wanaongeza plastiki kwenye mafuta wakati wa kukaanga chips za ndizi.
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Ghana imesema imeanza kufanya ukaguzi katika masoko pamoja na vipimo vya maabara ili kuchunguza madai ya uchafuzi wa chips za ndizi.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya video kusambaa mitandaoni ikionyesha watengenezaji wakidaiwa kuyeyusha plastiki aina ya Low-Density Polyethylene kwenye mafuta ya kukaangia.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, matumizi ya plastiki katika mafuta ya moto yanaweza kusababisha kemikali hatari kuingia kwenye chakula na kuhatarisha afya ya walaji.
FDA imeeleza kuwa itatoa matokeo ya uchunguzi huo baada ya vipimo vya maabara kukamilika.
CHANZO: Newstimehub
Comments
No comments Yet
Comment