Sport
Dollar
38,8949
0.36 %Euro
43,4533
-0.25 %Gram Gold
3.997,1000
-0.9 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mpangilio duni na msongamano wa vibanda na maduka zimesababisha visa vingi vya moto katika soko hili kubwa zaidi nchini Kenya na hasara ya mamia ya milioni ya pesa.
Wafanyibiashara wa nguo, viatu na mali zingine kuu kuu katika soka la Gikomba, jijini Nairobi wanahesabu hasara yao kwa mara nyingine baada ya moto wa asubuhi kuteketeza vibanda vyao na kuharibu mali ya mamilioni ya pesa.
Japo sababu ya moto huo bado haijabainishwa, maelezo ya awali ni kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa tisa usiku na kusambaa haraka kupitia sehemu ya viatu iliyo karibu na barabara ya Lamu eneo la Pumwani, Majengo.
Mbunge wa ene hilo Yusuf Hassan alithibitisha kisa hicho, na kusema kuwa wazima moto wa kaunti na watu wa kujitolea wa eneo hilo walijibu haraka kukabiliana na moto huo.
"Tunashukuru hatua za haraka zinazochukuliwa na huduma za dharura, lakini ni lazima tushughulikie sababu kuu za moto huu unaotokea mara kwa mara," alisema.
Hakuna majeruhi
Polisi walisema hakuna majeruhi au majeraha yaliyosababishwa moja kwa moja na tukio hilo.
Mpangilio duni na msongamano wa vibanda na maduka zimesababisha visa vingi vya moto katika soko hili kubwa zaidi nchini Kenya na hasara ya mamia ya milioni ya pesa.
Kisa cha hivi punde zaidi kilitokea Aprili 1 wakati moto mwingine ulizuka takriban saa 3:00 asubuhi katika sehemu ya Kwa Mbao sokoni.
Moto huo uliteketeza eneo lote na kusambaa hadi kwenye kituo cha mabasi jirani.
Comments
No comments Yet
Comment