Wakazi wa Bamako wanakabiliwa na changamoto kubwa baada ya makundi yenye silaha kuzuia njia za usafıri.

Makundi ya Kiislamu Yakaza Mzingiro Bamako, Raia Wakosa Njia za Kusafıri.

Wakazi wa Bamako nchini Mali wanakabiliwa na hali ngumu baada ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu kukaza mzingiro kuzunguka mji huo.

Taarifa zinaeleza kuwa barabara nyingi zinazoingia na kutoka mji huo zimewekwa vizuizi, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa usafıri wa abiria na mizigo,Baadhi ya wananchi wameshindwa kusafıri kwenda maeneo yao ya kazi au kurejea nyumbani, huku wakieleza hofu yao juu ya usalama wao na wa familia zao,Serikali imeongeza juhudi za kijeshi ili kufungua njia hizo na kurejesha hali ya kawaida, lakini bado changamoto kubwa ipo katika kudhibiti maeneo ya nje ya mji,

Wataalamu wa usalama wanasema kuwa hali hiyo inaonyesha kuongezeka kwa nguvu za makundi yenye silaha katika eneo hilo na changamoto inayokabili serikali katika kulinda miji mikubwa.

Chanzo:Newstimeshub 

#