Sport
Dollar
39,1462
-0.03 %Euro
44,7882
0.39 %Gram Gold
4.234,0400
0.29 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa sasa anayeondoka ni Lady Justice Imani Daud Aboud, raia wa Tanzania.
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu iliyo n amakao yake makuu jijini Arusha Tanzania inatarajiwa kuwachagua viongozi wapya katika kikao chao maalum cha 77.
Mahakama hiyo ya majaji 11 itafanya kura ya siri kuwachagua Rais na naibu wake wapya watakaoshika hatamu mpya ya miaka miwili, na wanaweza kuchaguliwa kwa mihula miwili pekee.
Rais wa Mahakama anakaa na kufanya kazi kwa muda wote kwenye kiti cha Mahakama, huku Majaji wengine kumi (10) wanafanya kazi kwa muda. Katika kutekeleza majukumu yake, Rais husaidiwa na Msajili ambaye anafanya kazi za Usajili, usimamizi na utawala wa Mahakama.
Mahakama ilianza shughuli zake rasmi mjini Addis Ababa, Ethiopia mwezi Novemba 2006. Mnamo Agosti 2007 ilihamia Arusha, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi wanaoondoka
Rais wa sasa anayeondoka ni Lady Justice Imani Daud Aboud, raia wa Tanzania.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu mnamo Julai 2018. Alichaguliwa tena kwa muhula wa pili na wa mwisho wa miaka sita (6) mnamo Februari 2021.
Alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama Rais wa Mahakama mnamo Mei 2021 na alichaguliwa tena Julai 2023, kwa muhula wa mwisho wa miaka miwili.
Naibu wa Rais ambaye ametumikia muhula mmoja ni Mhe. Jaji Sacko Modibo,raia wa Jamhuri ya Mali. Alichaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu mnamo Februari 2021, kwa muhula wa miaka sita. Alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Mahakama mnamo Julai 2023 kwa muhula wa miaka miwili.
Uundwaji wa mahakama hiyo
Mahakama hiyo ilianzishwa kwa mujibu wa Kifungu cha 1 cha Itifaki ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu kuhusu Uanzishwaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, (Itifaki) ambayo ilipitishwa na Nchi Wanachama wa Uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) huko Ouagadougou, Burkina Faso, mnamo Juni 2048.
Itifaki hiyo ilianza kutumika tarehe 25 Januari 2004.
Mataifa 34 ambayo yameidhinisha Itifaki hiyo ni: Algeria, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d’Ivoire, Comoro, Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea-Bissau, Kenya, Libya, Lesotho, Madagascar, Mali, Malawi, Msumbiji, Mauritania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Mauritius, Nigeria, Saudi Arabia, Nigeria, Mauritius, Mauritius, Mauritius Tanzania, Togo, Tunisia, Uganda na Zambia.
Kwa mujibu wa ukuasa wake mtandaoni , hadi sasa, ni nane (8) tu kati ya nchi thelathini na nne (34) Wanachama wa Itifaki ndio wameweka tamko la kutambua uwezo wa Mahakama kupokea kesi moja kwa moja kutoka kwa NGOs na watu binafsi.
Nchi hizo nane ni: Burkina Faso, Gambia, Ghana, Guinea-Bissau, Mali, Malawi , Niger na Tunisia.
Comments
No comments Yet
Comment