Liverpool ilipindua matokeo ya kufungwa 2-0 hadi kumaliza kwa ushindi wa 4-3 katika Uwanja wa Anfield,

Liverpool yapindua meza dhidi ya Villarreal kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Liverpool ilipindua meza baada ya kufungwa magoli mawili sifuri na kufanikiwa kumaliza kwa ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Villarreal siku ya Jumanne.

Timu ya Hispania ambayo ilikuwa ugenini na kuwashangaza wenyeji Liverpool katika Uwanja wa Anfield wakati Georges Mikautadze alipocheka na nyavu katika dakika nne.

Villarreal ikaongeza goli la pili katika dakika ya 29 kupitia Sergi Cardona.

Hata hivyo, Liverpool ikaanza kurudisha mapigo dakika saba baadaye kupitia Alexis Mac Allister.

Liverpool ilimaliza mechi hiyo kwa ushindi wa magoli 4-3.

#