Sport
Dollar
39,3377
0.38 %Euro
44,9062
-0.09 %Gram Gold
4.261,0600
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Tundu Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema akabiliwa na kesi kadhaa ikiwemo ya uhaini.
Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema, Tundu Lissu, imeanza kusikilizwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Lissu anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza taarifa potofu pamoja na kosa la uhaini. Kesi hiyo ni miongoni mwa zile zinazofuatiliwa kwa karibu na wadau mbalimbali ikiwemo wa haki za binadamu, vyombo vya habari, wanadiplomasia na wanasiasa kutokana na nafasi yake katika ulingo wa siasa nchini Tanzania.
Tundu Lissu, ambaye pia ni wakili na mwanasiasa mashuhuri, ameendelea kukanusha mashtaka dhidi yake akisisitiza kuwa yanachochewa kisiasa.
Mahakama imepanga kuendelea kusikiliza ushahidi kutoka kwa upande wa mashtaka katika vikao vijavyo.
Kesi hiyo inapeperushwa mubashara kupitia mtandao wa Mahakama ya Tanzania.
Wanaharakati kutoka Kenya na Uganda
Mei 19 ilikuwa ndio mara ya kwanza kwa kesi ya Tundu Lissu kusikilizwa ambapo pia ilihudhuriwa na baadhi ya wanaharakati kutoka nchini Kenya, huku baadhi ya waliotaka kuhudhuria kurudishwa wakiwa uwanja wa ndege, na wengine akiwemo Boniface Mwangi wa Kenya na Agather Atuhaire kutoka Uganda kukamatwa, na baadae kurudishwa nchini mwao.
Maombi ya siku saba
Wakati huo huo, mwanasiasa na kiongozi wa dini nchini Tanzania Josephat Gwajima, ametangaza kufanya maombi ya siku saba yatakayoambatana na kufunga kwa ajili ya kumuombea Tundu Lissu.
Comments
No comments Yet
Comment