Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini.
Baraza la Mawaziri la Kenya lililoketi Jumanne jioni, limeidhinisha uanzishwaji wa ofisi mpya za ubalozi Vatican City, Denmark na Vietnam.
Katika kikao chake kilichofanyika Ikulu ya Nairobi, baraza hilo limesema kuwa hatua ya kuanzisha balozi ndani ya Makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani, itakuza mahusiano kati ya mataifa hayo matatu.
“Uanzishwaji wa ubalozi wetu huko Vatican utaimarisha uhusiano wetu na taasisi za maendeleo za Kikatoliki ambazo zinaendesha jumla ya shule 7,700 na vituo vya afya 500 nchi nzima,” ilisomeka sehemu ya taarifa ya baraza hilo.
Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini.
Comments
No comments Yet
Comment