Sport
Dollar
38,7786
0.39 %Euro
43,8944
0.27 %Gram Gold
4.147,5900
1.06 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Wanadiplomasia wakuu wa Marekani, Saudi Arabia wanafanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa India na Pakistan katika jitihada za kupunguza hali tete inayoendelea kati ya nchi hizo
Wanadiplomasia wakuu wa Marekani na Saudi Arabia leo Jumamosi wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na wenzao wa India na Pakistan ikiwa ni sehemu ya jitihada za kujaribu kupunguza uhasama kati ya nchi mbili hizo baada ya kufanya mashambulizi ya kulipizana.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani Ishaq Dar alimuelezea mwenzake wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan bin Abdullah kuhusu hali ya sasa katika eneo hilo baada ya Pakistan kuanzisha Operesheni Bunyan-un-Marsoos, or Ukuta wa Chuma, iliyotumia makombora ya Al-Fatah ikiwa ni majibu ya mashambulizi ya kijeshi ya India dhidi ya Pakistna, imesema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia ametoa rambirambi zake kwa raia waliopoteza maisha na kushukuru hatua ya tahadhari ya Pakistan,” imesema taarifa hiyo.
Waziri wa Saudia wa Nchi wa Masuala ya Mambo ya Nje Adel Al-Jubeir pia aliitembelea New Delhi na Islamabad siku mbili zilizopita.
Al-Jubeir ametaka kupunguzwa kwa mashambulizi kati ya nchi hizo mbili zenye nuklia.
Alikutana na Waziri Mkuu wa Pakistani Muhammad Shehbaz Sharif Islamabad Ijumaa, siku moja kabla ya ziara yake ya ghafla ya New Delhi ambapo alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India S. Jaishankar.
Kando, Jaishankar amesema alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio Jumamosi.
"Mwelekeo wa India siku zote umekuwa wa tahadhari na wa uwajibikaji na utabaki kuwa hivyo," aliandika katika mtandao wa X.
Comments
No comments Yet
Comment