Sport
Dollar
41,1665
0.01 %Euro
48,0488
0.02 %Gram Gold
4.685,5100
-0.54 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais wa Ghana John Mahama amemfuta kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo Gertrude Torkonoo baada ya uchunguzi kubaini madai ya matumizi mabaya ya mamlaka yake.
Rais wa Ghana amemfuta kazi Jaji Mkuu wa nchi baada ya uchunguzi kubaini madai ya matumizi mabaya ya mamlaka.
Gertrude Araba Esaaba Sackey Torkonoo, 61, mwanamke wa tatu kuongoza mahakama kuu ya Ghana, alisimamishwa kazi katika nafasi yake hiyo aliyoingia 2023 baada ya malalamiko kadhaa kuwasilishwa dhidi yake.
Rais John Mahama aliteua tume ya wajumbe watano ikiongozwa na jaji mwingine wa mahakama ya juu kuchunguza madai hayo, ikiwemo yale ya kuwepo kwa rekodi za uwongo za mahakama na ubadhirifu wa fedha za umma.
Tume hiyo ilibaini kuwa madai hayo "yalikuwa ya kweli na kupendekeza aondolewe ofisini ," taarifa kutoka ofisi ya rais ilisema siku ya Jumatatu.
Mara ya kwanza kwa jaji mkuu kuondolewa ofisini Ghana
Comments
No comments Yet
Comment