Dollar

41,1661

0.01 %

Euro

48,0587

0.03 %

Gram Gold

4.702,5900

-0.17 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Chama hicho cha upinzani kimeendelea kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania, siku sita toka kuanza kwa kampeni za nchi nzima kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

CHAUMMA wajinadi na sera ya mabadiliko

Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) nchini Tanzania kimewaomba Watanzania kukipa ridhaa ya kuiongoza nchi hiyo, kwa ahadi ya kusukuma mbele vuguvugu la mabadiliko katika nchi hiyo.

Akizungumza mjini Morogoro, mgombea mwenza wa urais wa chama hicho, Devotha Minja amesema ni vyema watanzania wakakichagua chama hicho, ili kiharakishe ajenda ya mabadiliko na mageuzi.

Kulingana na Minja, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kukichagua CHAUMMA iki ikabili mifumo ya kodi ambayo si rafiki kwa wananchi.

“Kama CHADEMA hawapo, basi mtuunge mkono mkono kwa sababu adui yetu ni CCM, tunazitaka ‘reforms’…tukiingia bungeni itakuwa ni reforms, reforms, reforms. Hicho ndicho kitakachokuwa kipaumbele cha CHAUMMA,” alisema Minja.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#