Ripoti zatofautiana kuhusu chanzo cha kuanguka kwa F-15.

Iran yadai ndege ya kivita ya Marekani ilidunguliwa Kuwait

Vyombo vya habari vya Iran vimedai kuwa ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15 iliangushwa baada ya kushambuliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran, ingawa mamlaka za Kuwait na Marekani hazijathibitisha taarifa hiyo rasmi.

Video zilizosambazwa mitandaoni zinaonesha kinachodaiwa kuwa ndege hiyo ikiwa imeanguka pamoja na rubani akishuka kwa mwavuli kabla ya kuokolewa na raia waliokuwa karibu.

Hata hivyo, baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa huenda tukio hilo lilitokea kwa bahati mbaya, huku uchunguzi rasmi ukiendelea kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

CHANZO: Newstimehub

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#