Sport
Dollar
43,1251
-0.01 %Euro
50,4241
0.39 %Gram Gold
6.412,9700
2.59 %Quarter Gold
10.502,7600
0.98 %Silver
118,5900
7.14 %Mwanadiplomasia mwandamizi wa Iran anasema nchi yake inaangazia kuwa na makubaliano ambayo yanaheshimu haki za wote na usawa.
Majadiliano na Marekani yanawezekana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi alisema siku ya Jumatatu, hata wakati nchi yake ikisema iko tayari kikamilifu kwa vita.
Akizungumza na mabalozi wa nchi za nje mjini Tehran kupitia Televisheni ya Taifa, Araghchi alisisitiza kuwa Iran haitaki vita lakini iko tayari kujlinda dhidi ya mashambulizi.
"Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaki vita lakini iko tayari kikamilifu kwa vita," Araghchi alisema.
"Tuko tayari pia kwa majadiliano, lakini majadiliano hayo yanatakiwa kuwa ya usawa, yakiwa na haki sawa na kwa misingi ya kuheshimiana."
‘Njia thabiti’
Mapema Rais wa Marekani Donald Trump alisema uongozi wa Iran unataka mazungumzo baada ya kutishia kushambulia kijeshi kufuatia maandamano.
Trump alisema Jumapili kuwa serikali yake inafuatilia kwa makini hali ilivyo nchini Irn na inatafakari kuhusu "njia thabiti" huku idadai ya waliofariki kwenye maandamano yanayoendelea ikisemekana kuwa mamia ya watu.
"Jeshi linafanyia hali tathmini, na tunaangalia njia thabiti. Tutafanya maamuzi," Trump aliwaambia waandishi wa habari akiwa kwenye ndege ya rais wa Marekani ya Air Force One kuelekea Washington, DC, kutoka Mar-a-Lago, Florida.
Trump pia alisema amekuwa akipata taarifa za kila saa kuhusu Iran, bila kueleza zaidi kuhusu wakati gani, wapi, na namna gani Marekani itachukua hatua.
Maandamano ya Iran
Iran imekumbwa na maandamano tangu mwishoni mwa mwezi Disemba kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayokithiri.
Shirika la haki za binadamu lenye makao yake nchini Marekani la HRANA linasema waliofariki ni waandamanaji 490 na maafisa wa usalama 48, huku watu zaidi ya 10,600 wakikamatwa, ingawa hakuna makadirio rasmi kuhusu idadi hiyo.
Mwezi Juni mwaka uliopita, Marekani ilishambulia maeneo matatu ya kutengeneza nyuklia ya Iran — Fordow, Natanz, na Isfahan — ikiwa ni sehemu ya operesheni yao ya Midnight Hammer wakati wa vita vya muda mfupi vya Iran na Israel.
Pamoja na kutoa onyo kuhusu hatua za kijeshi, Trump amesema anaangalia njia za kurejeshwa kwa huduma za mtandao Iran huku zikiwa zimekatishwa kote, akisema kuwa atazungumza na Elon Musk kuhusu hilo.
Comments
No comments Yet
Comment