Dollar

40,1836

0.22 %

Euro

47,1110

0.05 %

Gram Gold

4.333,1200

1.15 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Akiwa Arsenal, hakusifika tu kwa upachikaji wake wa mabao, bali alitambulika kama mchezaji mwenye mguu mkubwa zaidi, akivaa kiatu saizi 15.

Gwiji wa Arsenal na Nigeria: Nwankwo Kanu

Anaitwa Nnwanko Kanu, ‘ngongoti’ kutoka mji wa Oweri nchini Nigeria, aliyekuwa sehemu ya kikosi cha ‘Invicibles cha mzee Arsene Wenger, pale Arsenal.

Akiwa amejijengea heshima na historia yake ya kipekee pale Highbury, akiwa pia amechezea klabu mbalimbali zikiwemo Ajax, Inter Milan, West Bromwich Albion, na Portsmouth.

Kanu, ambaye alijizoelea umaarufu kwa staili yake ya kushangilia kwa kupiga saluti kwa vidole viwili, ni kati ya waafrika waliowahi kubeba taji la Klabu Bingwa Ulaya, UEFA Super Cup na medali ya dhahabu Olimpiki, akiwa na akina Celestine Babayaro, fundi Jay Jay Okocha na mchungaji Taribo West.

Alizaliwa miaka 48, na kipaji chake kilianza kuonekana akiwa chalii tu wa miaka 17.

Alijiunga na Ajax Amsterdam ya Uholanzi mwaka 1993, akitupia nyavuni mabao 25 ndani ya michezo 54.

Miaka 3 baadaye, Kanu alihamia ligi kuu ya Italia, maarufu kama Seria A, akisajiliwa na Fogo wa Inter Milan ya wakati huo, Massimo Moratti.

Kanu alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria, maarufu kama ‘Super Eagles’ kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka 1996 jijini Atlanta Marekani, kikosi ambacho kiliushangaza ulimwengu kwa kuwatoa Brazil kwenye hatua ya Nusu Fainali na kutwaa medali ya dhahabu.

Furaha ya kutwaa dhahabu, nusura ikigeuke huzuni kwa wapenda soka wa Afrika na ulimwenguni kwa ujumla, baada ya fowadi huyo kugundulika maradhi hatari ya moyo, ambayo yalitishia uhai wake.


Taarifa hizo zilimshtua bosi wa Inter, mzee Moratti ambaye aliamua kulivalia njuga suala lake la matibabu ya Kanu, na kumuwezesha kurejea tena uwanjani baada ya kufanyiwa upasuaji mwaka 1997.

Miaka miwili baadaye, Kanu akasafiri hadi kaskazini mwa jiji la London, na kujiunga na Arsenal.

Mwaka huo huo, Kanu akiwa na mtindo wake wa ‘panki’ kichwani, akachaguliwa kama  mchezaji bora barani Afrika kwa mara ya pili.

Ndani ya Arsenal, Kanu alikuwa na bahati ya kucheza pamoja na nyota wengine wakiwemo Thierry Henry na Dennis Bergkamp.

Atakumbukwa kwa kutupia ‘hat-trick’ kwenye mechi dhidi ya Chelsea, mwaka 1999.

Ameichezea Arsenal jumla ya michezo 197, akipachika nyavuni magoli 44.

Japo aliondoka Arsenal mwaka 2004, kuelekea West Bromwich Albion, ngongoti huyo alishiriki kwenye mchezo maalumu wa kumuaga Dennis Bergkamp mwaka 2006, katika mchezo uliofanyika uwanja wa Emirates.

Bado mashabiki wa Arsenal wanaendelea kuliimba jina la Kanu, kila mara anapofika Emirates.

Kimataifa, Kanu alitundika daluga zake baada ya Nigeria kuondolewa kwenye Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010, akiwa ameichezea ‘Super Eagles’ mechi 86 na kutupia mabao 12.

Mwaka 2022, alichaguliwa kama mchezaji bora wa Nigeria wa muda wote.

Ameanzisha taasisi yake ya Moyo na kujenga hospitali kwa ajili ya kutibu watoto wenye matatizo ya moyo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#