Gambia imekabiliwa na maandamano katika wiki za hivi karibuni kutokana na kukatika kwa umeme na maji.

Gambia yanunua majenereta mawili makubwa kukabiliana na tatizo la umeme

Gambia imepata majenereta mawili mapya yenye uwezo wa megawati 21 kukabiliana na tatizo la umeme.

Tangu Juni, Gambia imekuwa ikikabiliwa na kukatika kwa umeme, ambapo hali hiyo imekuwa mbaya zaidi katika wiki za hivi karibuni.

Majenereta hayo, yenye uwezo wa megawati 10.5 kila moja, yalifika siku ya Jumatatu katika bandari ya mji mkuu Banjul kutoka China, yalikoagizwa.

Mpango wa kudumu

"Kuwepo kwa majenereta hayo ni sehemu ya suluhu kwa matatizo ya umeme. Serikali inataka kuweka kama sehemu ya mpango wa sasa na wa kudumu kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linatatuliwa kabisa," Makamu wa Rais Muhammed Jallow alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maji na Umeme la Gambia anasema majenereta hayo yatafungwa kufikia mwisho wa mwezi huu.

"Mashine hizo hazijawahi kutumika, inachohitajika ni kuyafunga sasa," Gallo Saidy amesema.

#