Sport
Mdhibiti wa mawasiliano asema maudhui ya chuki na taarifa za uongo zinachochea mgawanyiko na kutishia taasisi za serikali.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Gabon imetangaza kusimamishwa kwa matumizi ya mitandao ya kijamii hadi itakapotolewa taarifa nyingine. Msemaji wa taasisi hiyo alisema hatua hiyo inalenga kudhibiti maudhui ya chuki, matusi na taarifa potofu ambazo zimekuwa zikichochea mgawanyiko katika jamii.
Kwa mujibu wa mdhibiti huyo, kuenea kwa taarifa zisizo sahihi, unyanyasaji mtandaoni na uvujaji wa data binafsi kumeathiri utulivu wa taasisi za serikali na kuhatarisha maendeleo ya kidemokrasia. Hata hivyo, mamlaka imesisitiza kuwa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni bado ni haki ya msingi inayolindwa kisheria nchini humo.
Hatua hiyo inakuja wakati Rais Brice Oligui Nguema akikabiliwa na wimbi la kwanza la maandamano tangu aingie madarakani mwaka jana. Walimu wamekuwa wakigoma tangu Desemba wakidai kuboreshwa kwa mishahara na mazingira ya kazi, huku maandamano yakienea katika sekta nyingine za umma kama afya, elimu ya juu na vyombo vya habari.
Chanzo: Africanews
Comments
No comments Yet
Comment