Dollar

40,6894

0.04 %

Euro

47,1293

0.03 %

Gram Gold

4.411,9000

-0.21 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

‘Simba wa Teranga’ wamewathibitishia ‘Tai wa Kijani’ kuwa wao ni bora kwa kiwango cha soka duniani, baada ya kuilaza kwa bao 1-0, katika mchezo wa Kundi D wa michuano ya CHAN 2024.

CHAN 2024: Senegal yaibuka mbabe dhidi ya Nigeria

Bao la dakika ya 75 lililofungwa na Christian Gomis, limeipa Senegal alamu tatu muhimu, katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi D, uliofanyika katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Wakitumia mfumo wa 4-4-2, Senegal waliuanza mchezo huo kwa kasi, wakikabiliana na rafu kutoka kwa wachezaji wa Nigeria.

Hata hivyo, mchezo huo ulianza kupooza ilipofikia dakika ya 15 ya mchezo, huku timu zote zikishindwa kufanya mashambulizi ya maana kwenye ngome za wapinzani wao.

Dakika 20 baadaye, Nigeria walifanikiwa kuudhibiti mchezo, kwa pasi za ‘kampa kampa tena’, wakijaribu kutengeneza nafasi za mashambulizi dhidi ya ‘Simba wa Teranga’.

Hadi mwisho wa kipindi cha kwanza, hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kidogo, na baada ya kosakosa za hapa na pale na kukamiana, kabla ya Christian Gomis kuizawadia  Senegal bao la pekee katika mchezo huo, kupitia kwa Christian Gomis.

Kazi nzuri iliyofanywa na Koité, akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya Nigeria, kabla ya kumtengea Gomis, ambaye bila hiyana alitumbukiza wavuni.

Wakati huo huo, Congo na Sudan zilitoka suluhu ya 1-1, katika mchezo mwingine wa Kundi D, uliofanyika kwenye uwanja wa Amaan.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#