Sport
Dollar
40,6715
0.07 %Euro
46,5137
0.01 %Gram Gold
4.304,7500
0.12 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Ottawa inapanga kuitambua Palestine katika Umoja wa Mataifa Septemba 25 iwapo Mamlaka ya Palestina inazingatia utawala bora na kuwaondoa Hamas katika uongozi ujao
Canada imetangaza kulitambua Taifa la Palestina katika mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 2025-kwa masharti kwamba Mamlaka ya Palestina itafanya mabadiliko muhimu na kutahadharisha kwamba uwezekano wa suluhu ya mataifa mawili “inafutwa mbele ya macho yao.”
“Canada imekuwa ikiunga mkono suluhu ya mataifa mawili-taifa la Palestina lililo huru linaloishi pamoja na Taifa la Israel kwa amani na utulivu,” amesema Waziri Mkuu Mark Carney katika taarifa yake.
“Kwa miongo kadhaa, ilitarajiwa kwamba matokeo haya yangefikiwa kama sehemu ya mchakato uliojengeka kupitia majadiliano kati ya serikali ya Israel and Mamlaka ya Palestina. Kwa masikitiko, mtazamo huu haupo tena.”
Carney ameelezea mambo kadhaa ambayo yamerudisha nyuma mchakato wa amani, ikiwemo kuongezeka kwa upanuzi wa makazi ya Israel katika eneo linalokaliwa la West Bank na Mashariki mwa Jerusalem, hatua ya bunge la Israel kuongeza sehemu ya West Bank iliyokaliwa, na janga la kibinadamu Gaza huku kukiwa na zuio la msaada kufika.
“Mateso ya raia hayatoi fursa ya kucheleweshwa kwa hatua ya kimataifa,” Carney amesema.
Kuitambua kunategemea mabadiliko
Canada kuitambua Palestina kutategemea mabadiliko yatakayofanywa na Mamlaka ya Palestina.
Hii ikiwemo ahadi ya Rais Mahmoud Abbas ya kufanya uchaguzi ifikapo 2026 ambapo Hamas hawatashiriki, na kuhakikisha kuwanyang’anya silaha.
Carney pia ametaka kuachiliwa haraka kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas tangu Oktoba 7, kundi hilo kunyang’anywa silaha, and kutokuwa na jukumu lolote katika kuongoza Palestina.
“Canada siku zote itaunga mkono uwepo wa Israel kama taifa huru katika Mashariki ya Kati kwa kuishi kwa amani,” Carney amesema.
“Njia yoyote ya amani ya kudumu kwa Israel pia inataka kuwepo kwa taifa tulivu la Palestine, na ambalo linatambua haki ya Israeli ya amani na utulivu.”
Carney amesema, Canada itafanya kazi na wadau wa kimataifa kuja na mpango wa amani na kuhakikisha kiwango kikubwa cha msaada kinafikishwa Gaza.
“Canada atakuwa ni mshirika muhimu katika kujenga amani yenye usawa na ya kudumu katika eneo hilo-amani ambayo inaheshimu utu, ulinzi na malengo ya Wapalestina na Waisraeli.”
Comments
No comments Yet
Comment