Sport
Jean-Guy Blaise Mayolas amepatikana na hatia ya kutumia vibaya dola milioni 1.3 za ruzuku ya FIFA zilizotolewa wakati wa janga la COVID-19.
Mahakama imemhukumu kifungo cha maisha rais wa Shirikisho la Soka nchini Congo, Jean-Guy Blaise Mayolas, baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji fedha.
Kulingana na uchunguzi uliofanywa, fedha hizo zilikuwa ni msaada uliotolewa na FIFA kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya soka wakati wa janga la COVID-19.
Fedha hizo zilipaswa kutumika katika miradi ya maendeleo ya soka ikiwemo ujenzi wa viwanja na kukuza soka la wanawake nchini Congo.
Hata hivyo, wachunguzi walisema kiasi kikubwa cha fedha hizo kilielekezwa kwenye matumizi binafsi ya Mayolas, jambo lililopelekea yeye pamoja na familia yake kukutwa na hatia.
CHANZO: Newstimehub
Comments
No comments Yet
Comment