Sport
Dollar
43,3074
0.04 %Euro
50,8626
0.09 %Gram Gold
6.628,8300
0.16 %Quarter Gold
10.936,4100
0 %Silver
131,6200
0.38 %Mwaka 2022, Musk alitumia kiasi cha Dola Bilioni 44, kuununua mtandao wa Twitter, ambao aliubadilisha jina na kuuita X.
Bilionea namba moja duniani, Elon Musk amegusia kulinunua shirika la ndege la Ryanair, hatua iliyoibua majibizano kati yake na bosi wa shirika hilo, Michael O'Leary.
Musk, ambaye pia ni mmiliki wa wa mtandao wa X (zamani Twitter) na kampuni ya magari ya Tesla, kwa siku kadhaa sasa, amekuwa akionesha nia ya kuinunua kampuni ya ndege ya Ryanair, shirika kubwa la ndege barani Ulaya.
Katika hatua nyingine, Musk ametaka O'Leary's atimuliwe kazi na shirika hilo, huku akimuita ‘mpumbavu’.
Majibizano ya wawili hao, yalianza baada ya O'Leary kufanya mahojiano na redio moja ya nchini Ireland, ijulikanayo kama Newstalk.
Kupitia mahojiano hayo, O'Leary alipinga uwezekano wa kampuni ya Starlink inayomilikiwa na Musk, kutoa huduma za intaneti kwenye ndege zake, jambo ambalo litagharimu kiasi cha Dola Milioni 250 kwa mwaka.
“Abiria wa Ryanair hawatokuwa tayari kulipia huduma ya aina hii, Musk hafahamu chochote kuhusu usafiri wa anga, nitaendelea kupuuzia kila aina ya taarifa zake potofu kwenye mtandao wake wa X," alisema.
Mwaka 2022, Musk alitumia kiasi cha Dola Bilioni 44, kuununua mtandao wa Twitter, ambao aliubadilisha jina na kuuita X.
Comments
No comments Yet
Comment