Dollar

43,1964

0.01 %

Euro

50,2832

0.01 %

Gram Gold

6.404,3900

0.15 %

Quarter Gold

10.585,2500

0 %

Silver

128,2500

0.42 %

Misri na mataifa mengine matatu yalifanya juhudi kubwa za kidiplomasia wiki hii kuishawishi Marekani isifanye shambulio dhidi ya Iran, kulingana na afisa mmoja kutoka eneo la Ghuba aliyeliambia shirika la habari la Reuters.

Misri na nchi nyingine tatu zimemshawishi Trump kutoishambulia Iran: Reuters

Mataifa hayo manne yalifanya diplomasia ya kina kati ya Marekani na Iran ili kuzuia shambulio lililotishia kufanywa na Marekani dhidi ya Iran, kufuatia hatua za Iran dhidi ya waandamanaji.

Saudi Arabia, Qatar, Oman na Misri zilihusika katika juhudi hizi za kidiplomasia kwa kipindi cha saa 48 kabla ya Rais wa Marekani Donald Trump kuashiria siku ya Alhamisi kwamba hatimaye alikuwa ameamua kutoishambulia Iran.

Afisa huyo alisema kuwa mataifa hayo manne yaliiambia Washington kuwa shambulio lolote lingeleta madhara makubwa kwa eneo zima, hasa katika masuala ya usalama na uchumi, ambayo hatimaye yangeliathiri pia Marekani. Afisa huyo alizungumza na shirika la habari la Reuters kwa masharti ya kutotajwa jina.

Aidha, waliiambia Iran kwamba shambulio lolote la kulipiza kisasi dhidi ya kambi za Marekani katika eneo la Ghuba lingekuwa na athari mbaya kwa uhusiano wa Iran na nchi nyingine za eneo hilo.

Kupunguza kauli kali

Ofisi ya vyombo vya habari ya kimataifa ya Saudi Arabia, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Wizara ya Habari ya Oman, pamoja na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri hawakutoa ufafanuzi wowote kuhusu suala hilo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), ambayo haikuhusika katika diplomasia hiyo kulingana na afisa huyo, nayo pia haikutoa ufafanuzi iwapo ilihusika katika juhudi zozote za kidiplomasia kuhusu suala hilo.

Gazeti la Wall Street Journal liliripoti wiki hii kuwa Saudi Arabia, Qatar na Oman zilifanya juhudi za kushawishi Marekani dhidi ya shambulio hilo.

Afisa huyo alisema juhudi za kidiplomasia zililenga kupunguza kauli kali na kuepuka hatua zozote za kijeshi ambazo zingesababisha machafuko makubwa zaidi katika eneo hilo. Aliongeza kuwa diplomasia hiyo huenda ikaishia kufungua njia ya mazungumzo kuhusu mgogoro wa mpango wa nyuklia wa Iran.

Kambi za kijeshi za Marekani katika Ghuba

Nchi za Ghuba zina hofu kuwa kambi za kijeshi za Marekani zilizopo katika nchi zao vinaweza kulengwa iwapo Iran italipiza kisasi dhidi ya mashambulio ya Marekani. Pia wana wasiwasi kuwa miundombinu ya nishati, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa eneo hilo, inaweza kulengwa.

Saudi Arabia na Qatar zina uhusiano mzuri na utawala wa Trump. Qatar na Misri pia zilihusika kwa karibu na Marekani katika juhudi za upatanishi kuhusu vita vya Israel dhidi ya Gaza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#