Akifunga mafunzo ya maafisa na askari uhifadhi 239, Kamishna wa Uhifadhi, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Massana Mwishawa amewataka wahitimu hao kuzingatia misingi hiyo katika utumishi wao.
Kamishna wa Uhifadhi, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Massana Mwishawa amesisitiza kuwa uzalendo, uadilifu, weledi na kuzingatia misingi ya sheria ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya uhifadhi na utalii.
Kamishna Mwishawa alitoa maelekezo hayo alipokuwa akifunga mafunzo kwa Maafisa na Askari Uhifadhi 239 waliohitimu mafunzo ya uongozi na kuwaelekeza kuzingatia misingi hiyo katika utumishi wao, wilayani Mlele mkoano Katavi
Wakati huo huo, Kamishna Mwishawa amewaelekeza wahitimu hao kutumia maarifa na ujuzi walioupata darasani na wakati wa mafunzo ya vitendo kuimarisha mshikamano na ushirikiano kazini, kusimamia haki na usawa, kupinga vitendo vya rushwa na kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo.
Mafunzo hayo yamewashirikisha Maafisa Uhifadhi 74 na askari uhifadhi viongozi 165 yakilenga kuimarisha misingi ya uongozi, nidhamu na uwezo wa kusimamia rasilimali za wanyamapori na misitu pamoja na kuboresha huduma kwa watalii.
