Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) walisema siku ya Jumatano kuwa mji mkuu Kaskazini mwa Sudan Darfur wa Al Fasher umeharibiwa na hakuna watu wanaoishi baada ya wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) kuwepo hapo kwa miezi kadhaa.
Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) walisema siku ya Jumatano kuwa mji mkuu Kaskazini mwa Sudan Darfur wa Al Fasher umeharibiwa na hauna watu baada ya wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) kuwepo hapo kwa miezi kadhaa.
Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wao, shirika hilo la misaada ya matibabu linasema linasema hivi karibuni liliruhusiwa kuingia Al Fasher japo kwa uchache kutathmini hali ya raia na vituo vya afya, ikiwa ni mara yake ya kwanza katika mji huo tangu kusitisha operesheni zake Agosti 2024.
MSF inasema maafisa wake walikuwa katika mji huo kwa saa nne tarehe 15 Januari chini ya uangalizi mkali wa maafisa wa usalama, wakieleza kuwa maeneo mengi yalikuwa yameharibiwa na mitaa haina watu kabisa.
“Mji huo sasa ni mahame, ” ilisema, ikiongeza kuwa idadi ndogo ya raia ndiyo wanaonekana kubaki katika eneo hilo au kurudi baada ya RSF kuchukua udhibiti mwezi Oktoba.
kumbukumbu mbaya
Maafisa wa MSF walienda katika maeneo mawili ambayo wanawake, watoto, na wazee wako huko. Katika vituo hivyo, walikumbana na wagonjwa wanaume karibu 20 waliokuwa na majeraha na kusisitiza utayari wao wa kuwapeleka kwa matibabu zaidi ikiwemo upasuaji katika maeneo amabayo MSF ina uwezo wa kufanya upasuaji.
Ingawa maafisa hao hawakupata muda wa kufanya tathmini kamili na iliyo huru, MSF inasema haikuona uhitaji mkubwa wa matibabu katika mji wote.
Shirika hilo linasema hilo linaonesha kumbukumbu mbaya ya uharibifu mkubwa Al Fasher, likionya kuwa huenda idadi kubwa ya raia wameuawa au kuondoka katika makazi yao.
Vita vibaya
Kufuatia kuchukua udhibiti wa RSF huko Al Fasher mwishoni mwa mwezi Oktoba, MSF inasema imekuwa ikijitahid kuwatafuta manusura Darfur na karibu na mpaka mashariki mwa Chad, ikiongeza kuwa wasiwasi bado upo kuhusu hali ya raia ambao bado walikuwa hai wakati mji huo ulipotwaliwa na RSF.
Tangu Aprili 15, 2023, jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF wamekuwa wakikabiliana katika vita. Mgogoro huo umesababisha mauaji ya maelfu ya watu na mamilioni wengine kuondoka katika makazi yao.
Comments
No comments Yet
Comment