Dollar

43,4293

0.07 %

Euro

51,8680

-0.03 %

Gram Gold

7.219,0500

-3.79 %

Quarter Gold

13.142,1300

5.74 %

Silver

153,0300

-5.81 %

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, kamanda wa vikosi vya AFRICOM wamekamilisha ziara yao nchini Ethiopia kwa kuangazia usalama katika kanda, ushirikiano wa kijeshi

Waziri Mkuu wa Ethiopia ajadili usalama, ushirikiano na maafisa waandamizi wa Marekani Addis Ababa

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed siku ya Jumatano alimpokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Christopher Landau, na Kamanda wa Vikosi vya Marekani Afrika (AFRICOM) Jenerali Dagvin Anderson kujadili uhusiano wa mataifa hayo mawili na ushirikiano wa kikanda, maafisa wa Ethiopia wamesema.

Abiy alieleza mazungumzo hayo kuwa yenye tija na yenye msingi wa kuheshimiana, kulingana na taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo.

Ujumbe wa Marekani pia ulikuwa na mikutano mingine na Waziri wa Ulinzi wa Ethiopia Aisha Mohammed, na Waziri wa Mambo ya Nje Gedion Timotheos, wakiangazia kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kijeshi.

Katika taarifa, Wizara ya Ulinzi ya Ethiopia inasema pande zote zimekubaliana kufanya kazi pamoja kulinda maslahi ya taifa na kuangazia changamoto za usalama katika kanda, ikiwemo juhudi za kukabiliana na ugaidi.

Ziara hii inakuja wakati Jeshi la Anga la Ethiopia likisherehekea miaka 90, sherehe ambazo zilihudhuriwa na maafisa wa Marekani.

Jenerali Anderson anasema ziara hiyo inathibitisha uhusiano wa muda mrefu kati ya Ethiopia na Marekani, na kusaidia kuunda mfumo ushirikiano wa usalama katika siku zijazo kwenye Pembe ya Afrika.

Mikutano hiyo inakuja huku kukiwa na juhudi za kuanzisha tena diplomasia katika kanda hiyo kufuatia barua ya Januari 16 kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump kwa Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi, akipendekeza kuanzishwa kwa mazungumzo kufuatia Bwawa kubwa la Ethiopia, mradi mkubwa zaidi wa nishati barani Afrika.

Kulingana na ripoti, barua hiyo -- ambayo pia ilitumwa kwa viongozi wa kanda -- ilipendekeza kuanzisha tena juhudi za upatanishi zenye lengo la kutatua tofauti za muda mrefu kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#