Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Afrika Kusini ni nchi ya kwanza ya Afrika kuongoza mkutano wa G20, ikiwa ni urais wa kupokezana kila mwaka tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuwapokeza Marekani.
Msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa, Vincent Magwenya, anasema Ramaphosa hatompokeza Balozi mdogo wa Marekani mkutano wa G20 baada ya Marekani kusisitiza kuwa haitohudhuria mkutano huo rasmi jijini Johannesburg.
Mapema Ikulu ya White House ilitoa taarifa fupi ikisema balozi wake mdogo mjini Pretoria angehudhuria hafla ya kupokezana kama taratibu tu mwishoni mwa mkutano wa G20 wikiendi.
Balozi mdogo ndiyo aliyekuwa amepewa jukumu hilo, akiwa ni cheo cha chini cha balozi au waziri. Kulingana na Makumbusho ya Kitaifa ya Diplomasia Marekani, bado cheo hicho kinatumika kama mkuu wa ujumbe wa Marekani katika maeneo ambayo Marekani hayana uhusiano mzuri wa kidiplomasia na nchi hiyo.
"Balozi au mwakilishi wa ubalozi nchini Afrika Kusini anakuwepo pale tu kuthibitisha kuwa Marekani itakuwa mwenyeji wa mkutano wa G20; watapokea jukumu hilo mwishoni mwa hafla yenyewe, hawatokuwepo hapo kushiriki katika mazungumo rasmi," Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt aliwaambia waandishi wa habari.
Comments
No comments Yet
Comment