Sport
Dollar
42,5704
0.08 %Euro
49,6355
0.14 %Gram Gold
5.764,1000
0.31 %Quarter Gold
9.520,4300
0.28 %Silver
79,9700
0.15 %Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, tarehe 7 Desemba 2025, alihutubia viongozi wa mashinani wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) katika eneo la Lango, na kutoa ujumbe mkali kwa wapinzani na wananchi.
Rais Yoweri Museveni, akizungumza katika shule ya upili ya Lango, aliwakumbusha wananchi wa Uganda, mchango wa chama chaka cha NRM katika kuleta amani nchini humo.
Rais Museveni alisema: “Na hawa watu wote wanaoipinga NRM, hakuna mtu aliyetoa mchango wowote katika kuleta amani. Kwa hiyo ninyi watu wa Lango lazima muwe makini sana. Huu si mzaha. Huwezi kwenda kuchezea Uganda. Uganda sio nchi ya kuchezea.”
Museveni pia aliongeza: “Sisi si watu wa kutumiwa. Wanafikiri tunaweza kuchezewa. Sisi ni waaminifu kwa undugu wetu wa chama, lakini bila shaka tunajua kupigana pia.”Museveni alitumia hotuba hiyo kutetea kile alichokitaja kama amani na uthabiti uliodumu kwa miongo kadhaa chini ya utawala wa NRM.
Aliwakumbusha machafuko na vurugu zilizokumba Uganda kabla ya 1986, akidai kuwa serikali yake ndiyo iliyoleta utulivu huo.
Kadiri Uganda inavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2026, kauli hiyo inaashiria hoja ya Museveni kwamba kuipinga NRM kunaweza kuhatarisha amani iliyopo. Wakati huo huo, wapinzani wanamlaumu kwa kukandamiza sauti mbadala, ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu.
Waangalizi wanasema matamshi haya yanalenga kuimarisha uungwaji mkono wa NRM, hasa katika eneo la Lango, na kuwaonya wanaoweza kuipinga serikali kwamba kufanya hivyo kunaweza kudhoofisha uthabiti wa taifa.
Comments
No comments Yet
Comment